Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani na Mwenyekiti kamati ya Sherehe wilaya Bi Hadija Nasri Ali Leo Marchi 3, 2022 amesisitiza kuwepo kwa vielelezo vya miradi yote iliyopendekezwa kukaguliwa kwa ajili ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa uhuru 2022 unaotarajiwa kufika Mkoa wa Pwani Mapema Mwezi Mei.
Akiendelea Mkuu huyo alisisitiza kuwa idara zote zipendekeze miradi yenye kuleta tija katika jamii.
Akizungumzia umuhimu wa sensa ya watu na makazi sambamba na zoezi linaloendelea la utambuzi na uwekaji wa vibao vya anuani za makazi Bi Hadija amewataka Watendaji wa Kata kushirikiana na Madiwani Kwa pamoja kufanikisha mazoezi haya ikiwa ni sehemu ya kurahisisha shughuli za maendeleo zinazopangwa na serikali.
Ujumbe wa Sensa mwaka 2022 "SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO SHIRIKI KUHESHABIWA, TUYAFIKIE MALENGO YA TAIFA"
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.