Kikao cha baraza la Ushauri la Wilaya ya Mkuranga kilifanyika jana tarehe 15.01.2018 katika ukumbi wa mikutano wa Felix Garden Mkuranga mjini kujadili mipango pamoja na shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanyika hapa wilayani. Akizungumza katika kikao hicho, mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto Sanga alitoa shukrani za dhati kwa wananchi wote wa Mkuranga kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa vyombo mbalimbali vya usalama wa raia na hivyo kufanikisha kudhibiti vitendo vya uhalifu vilivyokuwa vinaashiria kutoweka kwa amani katika wilaya. “Hivi sasa wilaya yetu ni salama na wananchi wote wanaendelea vizuri na shughuli zao za kiuchumi” Alisema!.
Aidha pamoja na hali hiyo ya utulivu, alisisitiza kuwa zuio la PikiPiki (Bodaboda) kutotembea baada ya saa 12:00 Jioni linaendelea kama ilivyoazimiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Aliwataka wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwafuatilia wageni wote wanaoingia katika maeneo yao kwa kutambua wanapotoka na shughuli wanazozifanya. Pamoja na nasaha zake kwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho, Mhe. Mkuu wa wilaya alitoa matangazo yafuatayo:-
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.