Benki ya NMB Mkuranga Mkoa wa Pwani yatoa msaada wa vifaa vya ujenzi na nyenzo za kufundishia katika kijiji cha Kiparang'anda kilichopo kata ya Kiparang'anda
Akizungumza katika halfa ya shukrani Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Khadija Nasri Ali amewashukuru Benki ya NMB kwa kuwapatia msaada huo ambao unaenda kuendeleza ujenzi wa zahanati ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi, fedha kutoka Halmashauri sambamba na Serikali kuu ambayo imeleta fedha kiasi cha shilingi milioni 54 kwa ajili ya umaliziaji.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewapongeza NMB kwa namna ambavyo wamekua wadau wa maendeleo na kuwaomba kuendeleza ushirikiano katika kutekeleza miradi mbali mbali ikiwa ni sehemu yao ya kurudisha shukrani kwa jamii kupitia asilimia moja ya faida inayotokana na uendeshaji wa Taasisi hiyo.
Bi. Khadija alienda mbali zaidi kwa kuwapongeza Viongozi na wananchi wa Kijiji cha Kiparang'anda huku akiwasisitiza kuzidi kushirikiana katika kuimarisha ujenzi wa miundo mbinu ndani ya kijiji chao huku akiwataka vifaa walivyopewa na NMB vitumike vizuri ili kuhakikisha kituo hiko kinamalizika.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi Mwanamsiu Dosi amewashukuru NMB kwa kuweza kuwapatia msaada wa vifaa hivyo vya ujenzi ambavyo vimeipunguzia Halmashauri gharama ambapo fedha zilizopangwa kununua mabati zitaenda kuongeza nguvu kwenye miradi mingine.
Diwani wa Kata ya Kiparanganda Mhe.Shomari Mwambala ametoa shukurani kwa niaba ya uongozi wa kijiji cha Magoza pamoja na wananchi wote kwa Benki ya NMB kwa kuweza kuwasaidia katika kuweka juhudi katika kituo cha afya cha Kiparang'anda na kuahidi wao kama viongozi watazidisha juhudi na vifaa vilivotolewa vitatumika vizuri katika ujenzi.
Meneja wa Kanda wa NMB Bw Donatus Richard ameshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kupokea Misaada hiyo huku akiahidi kuendele kutoa sawa na mahitaji, jumla ya mabati 210, misumali kilo 40 na kompyuta tatu zimetolewa kwa lengo la kuunga juhudi za Mh. Rais za kuimarisha miundo mbinu ya Elimu na Afya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.