Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng Evarist Ndikilo ametangaza rasmi kuanza kwa mnada wa korosho Mkoani Pwani ambapo unatarajia kuanza tarehe 8/11/2017.
Ndikilo aliyasema hayo hapo Jana kwenye kikao cha wadau wa korosho wa Mkoa wa Pwani kilochofanyika wilayani Mkuranga ambapo kikao hicho kilihusisha wadau wa korosho kutoka wilaya zote za Mkoa wa Pwani.
Aidha Ndikilo aliwataka wale wote wanaohusika na maandalizi kwa ajili ya uuzaji na ununuzi wa korosho wafanye maandalizi mapema.
"Wanunuzi wa korosho wanatakiwa wakamilishe malipo yao ndani ya siku saba
na endapo mnunuzi huyo hatafanya hivyo mizigo yake yote ya korosho itakamatwa mpaka pale atakapolipa deni lake" Ndikilo alisema.
Ndikilo pia aliongeza kwa wale watu wote watakaohusika na udanganyifu wa aina yoyote kama vile udanganyifu kwenye ubora na kilo za korosho atawachukulia hatua za kisheria.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh Filberto Sanga amewataka wahusika wanaoratibu upatikanaji wa magunia kwa ajili ya kuhifadhia korosho yaani Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Pwani (CORECU) kuhakikisha magunia kwa Wilaya ya Mkuranga yanapatikana mapema kwani mpaka sasa wakulima wengi wameokota korosho na kupeleka majumbani mwao pasipo kuhifadhi kwenye magunia.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.