Mratibu TASAF Wilaya ya Mkuranga amewapa mafunzo Wasimamizi ngazi ya jamii (CMC) katika ukumbi wa Mwinyi Sekondari.
Mafunzo hayo yamefanyika October 24,2024 yenye lengo la kuwafundisha CMC taratibu za kufuata wakati wa manunuzi ya vifaa vya mradi wa ajira za muda mfupi kwa walengwa.
Aidha (CMC) walipatiwa mafunzo ya manunuzi ngazi ya jamii (community level) ambapo miradi hii itatekelezwa kwa kipindi cha Mwaka 1 ni ajira za muda mfupi ambapo utekelezaji wake unategemea nguvu kazi za walengwa wenye umri kuanzia miaka 18 - 65 watabuni miradi itakayosaidia jamii zao na baada ya utekelezaji miradi hii itasimamiwa na serikali ya vijiji vyao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.