Mratibu TASAF Mkoa wa Pwani Bi.Roseline Kimaro amefanya ziara katika Kata ya Mkamba na Kisegese na kutembelea katika Kijiji cha Kizapala,Kijiji cha Vianzi,Kibesa,Chamgoi na Kisegese.
Ziara hiyo imefanyika November 5,2024 ikiwa na lengo la kujionea jinsi zoezi la malipo ya walengwa linavyofanyika pamoja na kuzungumza nao juu ya miradi iliyoibuliwa.
Bi.Roseline Kimaro amewataka walengwa kuwa na ushirikiano ambao utawainua kiuchumi katika vikundi walivyovianzisha vya kuweka na kukopa kupitia vikundi hivyo waungane waweze kupata mradi wa pamoja utakaoleta mabadiliko ya kubadilisha Kaya zao.
Aidha amewataka Kaya ambazo zipo katika mradi wa (PWP) ambao unatoa ajira za muda wa miezi (6) wafanye kazi kwa bidii kupitia miradi ambayo jamii watakwenda kunufaika nayo na watakwenda kuongeza vipato katika Kaya zao kupitia malipo ya ujira wa kazi watakazofanya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.