Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2017 ulipita wilayani Mkuranga tarehe 04.06.2017 ukitokea wilaya ya Rufiji na baadae ulikabidhiwa wilaya ya Kisarawe tarehe 05.06.2017.
Mwenge wa uhuru wa mwaka 2017 umepitia miradi 8 ya Maendeleo katika sekta ya Maji, Afya, Ujasiriamali, Elimu, Uwekezaji, Utawala Bora na Kilimo yenye thamani ya shilingi bilioni 24,714,462,640.00 kati ya hizo shilingi 161,784,700.00 zimetoka Serikali kuu na shilingi 40,699,147.00 ni michango ya Halmashauri ya Wilaya. Nguvu za wananchi ni shilingi 89,895,000.00 na shilingi bilioni 24,422,083,793.00 ni mchango wa wadau wa maendeleo.
Kwa kuzingatia ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru 2017 wenye kauli mbiu isemayo “Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi yetu” uongozi wa Wilaya umeweka mikakati ya kushirikiana na sekta binafsi katika kuanzisha viwanda 56. Kati ya hivyo viwanda vidogo na vya kati 48 na viwanda vikubwa 8. Viwanda hivi vinazalisha bidhaa na kutoa ajira kwa wafanyakazi 4,977 ambapo kati ya hao wanaume ni 2,844 na wanawake 2,133. Viwanda 14 vinaendelea kujengwa, vipo katika hatua mbalimbali. Aidha kiwanda cha kutengeneza chumvi Neelkant Ltd ni moja ya miradi inayotekeleza dhana ya uchumi wa viwanda iliyozinduliwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.