Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu Charles kabeho ameiasa jamii kutimiza wajibu wa kushirikiana na wadau na Serikali kuwekeza katika elimu pamoja na kutatua changamoto hasa ya Miundombinu iliyopo kwenye baadhi ya shule.
Aidha amewaonya watu watakaobainika kudanganya katika kupata mikopo ya elimu wakati wana uwezo.
Kabeho alitoa rai hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mkuranga,Alisema kuna watu wenye uwezo wa kifedha lakini wanataka kudanganya ili wapate mikopo hiyo.
Kabeho aliwaagiza viongozi kuhakikisha baadhi yao waliobahatika kupata mikopo hiyo warejeshe haraka ili wengine wenye mahitaji wapate kunufaika na mikopo hiyo.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwennganyifge alieleza watakaobanika kudanganya ili kupewa kwa kufanya danganyifu wachukuliwe hatua za kisheria na kwamba serikali haipo tayari kuona hali kama hiyo inajitokeza.
Akizungumza Suala la wananchi kushirikiana na Serikali na wadau katika kuwekeza kwenye elimu alisema,licha ya mpango wa elimu bila malipo lakini wananchi wanapaswa kuwa sehemu ya kuchangia mahitaji muhimu ya watoto wao mashuleni.
Kabeho alibainisha ili kupunguza changamoto ya uhaba ya miundombinu hasa madarasa ni lazima kushirikiana kwa lengo la kupunguza tatizo la mrundikano wa wanafunzi katika baadhi ya shule.
“Ni jukumu la wananchi pia kuwezesha watoto wao katika mahitaji mengine kama sare za shule,chakula na madaftari” alisisitiza.
Pamoja na hayo alieleza kwamba hadi sasa wameshakimbiza mwenge huo katilmashaurika mikoa 20 na Halmashauri 104.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh.Filberto Sanga alisema kwamba Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Mkuranga utapitia miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya Tshs 2,675,776,900/-ambapo katika fedha hizo Serikali kuu imechangia Tshs 400,000,000/- Michango ya Wananchi Tshs 15,295,000/-,Halmashauri ya Wilaya Tshs 99,911,900/- na Wahisani walichangia Tshs 2,160,570,000/-
Mwenge wa Uhuru umeingia MkoaniPwani July 12 na utapitia miradi ya maendeleo 67 yenye thamani ya Tshs bilioni 162,440.8.Ambapo kati ya miradi hiyo 16 itawkewe mawe ya msingi,miradi 13 itazinduliwa,miradi 8 itafungliwa na 21 itakaguliwa.
Akikabidhiwa Mwenge huo Wilayani kuranga Ndikilo alisema Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani humo pia utapitia Wilaya 7 na Halmashauri 9.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.