Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhe. Mohamed Mwera amewaasa wakulima kuongeza thamani kwenye mazao ili waweze kupata masoko na bei nzuri itakayowapatia Tina. Mhe. Mwera ameyasema hayo leo Agosti 8, 2022 alipotembelea banda la maonesho la Halmashauri hiyo lililopo katika viwanja vya J.K Nyerere Mjini Morogoro na kupokea maelezo kutoka kwa Mkulima Julius Kibatega juu ya bidhaa zinazotokana na mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na viazi lishe, Muhogo na Chikichi. "Yapo mataifa yanayonufaika na uzalishaji mafuta ya kupika kwa kutumia zao la chikichi hivyo nyinyi wakulima mnatakiwa kutumia mbegu bora zinazozaliswa na wataalamu wa Halmashauri ya Mkuranga ili kilimo kilete tija na kiwe kinaonesha uhalisia halisi wa kauli mbiu ya mwaka huu inayosema ajenda 10/30 kilimo biashara,” alisema Mhe. Mwera. Nae Mkulima wa zao la korosho Bw. Seif Luaga alimuomba mwenyekiti huyo kusimamia upatikanaji wa “barcode” na mtaalam kutoka taas
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.