Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe.Abdallah Ulega amefanya Bonanza Maalum la kuhamasisha umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi katika Wilaya yake.
Katika Bonanza hilo ilifanyika Jogging maalum ya kujenga mwili ilianzia katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiguza na kumalizika katika viwanja vya shule ya Msingi Mkuranga.
Mhe.Ulega aliweza kuwapa vijana wote Jezi maalum pamoja na mipira kwa kila kikundi cha Jogging
Nae Mhe.Hadija Nasri Ali Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga ambae alihudhuria katika bonanza hilo amewataka vijana kuwa mabalozi wa kuweza kuhamasisha umuhimu wa Sensa ya watu na makazi katika maeneo waliyotoka ili Mkuranga ipae kimaendeleo tunatakiwa tujitokeze katika kuhesabiwa ili Serikali iweze kupata idadi kamili na kutupa mahitaji kamilifu.
Aidha amewataka kuwapa ushrikiano kamilifu kwa makarani wa sensa watakaopita katika maeneo yao na ikijitokeza kama kuna mtu hatokuwepo katika makazi yake basi aache taarifa zake kamilifu kwa atakaebaki.
Mhe.Ulega amewataka vijana kuzidi kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan na pia kuwaunga mkono Madiwani pamoja na Viongozi wetu wote ili tuzidi kusonga mbele katika kuleta maendeleo.
Amewashukuru sana kwa kuweza kijitokeza kwa wingi katika Bonanza hilo na kuwataka waweze kushiriki vizuri katika zoezi la sensa na kuwahamasisha wengine juu ya umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi katika Wilaya yetu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.