Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameupongeza uongozi wa serikali na taasisi wezeshi ndani ya Wilaya ya Mkuranga kwa kuweka mazingira rafiki na kuondoa urasimu kwa wawekezaji hali inayochangia viwepo viwanda vya mfano ndani na nje ya nchi
Akizungumza na wataalamu viongozi , wafanyakazi na jamii badala ya kutembelea kiwanda cha maji cha COOL BLUE kinachoendeshwa na SUPER MEAL LIMITED kilichopo kitongoji cha mwajasi kijiji cha Vianzi, Ndikilo alitumia fursa hiyo kupongeza mahusiano ya kitongoji ,kijiji na mwekezaji hali inayochangia kuondoa migogoro huku akiagiza Halmashauri zote ziige ubunifu huo.
Kwa upande wa bara bara Mhandisi Ndikilo alimpongeza kaimu wa Mratibu wa wakala wa bara bara mijini na vijijini(TARURA) Mkoa wa Pwani ambaye pia anaongoza Mkuranga Mhandisi Peter Shirima kwa kuitengea bajeti barabara hiyo huku akimwagiza Afisa Tarafa na watendaji wake wahamasishe wananchi kukata bure minazi yao ili kuepuka athari za umeme kiwandani na hata majumbani mwao
Akisoma taarifa Mkurugenzi wa kiwanda Faudhia Abdallah alisema wapo kwenye mchakato wa kujenga kiwanda cha juisi sambamba na kumalizia zahanati ya kijiji cha Vianzi walipo ili kudumisha mahusiano na wananchi
Ndikilo alimhakikishia Mkurugenzi wa kiwanda hicho kuwa ofisi yake na ya Mkurugenzi wa Halmashauri ipo tayari kuzisikiliza changamoto zao na kuzitatua kwa wakati ili kusimamia kauli ya Mh. Raisi Dk. John Pombe Magufuli ya kuwa na Tanzania ya viwanda
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.