.
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wakuu wa Udara ya kilimo na maafisa ugani wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanakua karibu na wakulima ili kuwapa elimu juu ya kilimo cha kisasa cha zao la muhogo.
Akizungumza katika kijiji cha Mkenge Kata ya Beta Wilaya ya Mkuranga mara baada ya kupokea taarifa ya kiwanda cha kuchakata muhogo) kinachoendeshwa na Tanzania Huafeng Agriculture Development Limite, Ndikilo alimpongeza Mmiliki wa kiwanda bwana Jie Qi (Jerry) kwakuwekeza sh.billioni 9.1 kwenye kiwanda hicho.
Akizungumzia changamoto mbali mbali Ndikilo alimwagiza meneja umeme Tanesco wilaya Octavian Mmuni, kuhakikisha swala la umeme kwenye kiwanda hicho linakua la uhakika ili kuepusha kukwama kwa uzalishaji wa malighafi hiyo.
Aidha Mhandisi Ndikilo alimuagiza kaimua katibu tawala Mkoa Shangwe Twamala kuitisha mapema kikao cha wadau wa muhogoili kweza kupanga mikakati itakayowezesha upatikananji wa tani 200 za mihogo kwa siku ili kuwezesha kiwanda kufanya kazi
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde alitumia fursa hiyo kumhakikishia Mkuu huyo watatumia Baraza lijalo la Madiwani kufikia muafaka kuhusu vituo vya kukusanya muhogo na uuzaji wake kupitia Chama cha msingi cha ushirika (AMCOS) hatmaye wakulima wafaidike sambamba na Halmshauri ya Wilaya.
.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.