Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng Evarist Ndikilo amewaagiza wakurugenzi wote wa Mkoa wa Pwani kutumia nishati mbadala badala ya mkaa ili kupunguza gharama.
Ndikilo aliyasema hayo leo hii kwenye kilele cha wiki ya Mazingira duniani kilichofanyika katika kijiji cha kisemvule kata ya Vikindu Wilayani Mkuranga.
"Natoa maelekezo kwa wakurugenzi kwamba Taasisi zote zinazotumia mkaa kwa wingi waone namna ya kutumia nishati mbadala,Tuone namna ya kubadilisha ili watumie gesi ili kuweza kuokoa ukataji wa miti na matumizi ya mkaa" Ndikilo alisema
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Eng.Mshamu Munde alisema "Tunapoharibu mazingira kwa kukata hovyo miti tutakosa mahali pazuri pa kuishi hata kwa viumbe hai wengine"
Munde aliongeza kwamba matumizi ya mkaa yanatakiwa kuachwa kwa kuacha ukataji wa miti na badala yake itumiwe nishati mbadala kama gesi asilia,umeme wa jua na makaa ya mawe.
Kilele cha siku ya mazingira Duniani kitaifa yanafanyika Mkoani Dar es salam na katika Mkoa wa Pwani maadhimisho haya yamefanyika katika wilaya ya Mkuranga Katika kijiji cha Kisemvule ikiwa na kauli mbiu isemayo"Mkaa ni gharama,Tumia Nishati mbadala"
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.