Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amefanya ziara Wilayani Mkuranga na kuzindua zoezi la uwashaji umeme katika vijiji vya Msufini Kidete na Hoyoyo katika kata za Mbezi na Tengelea wilayani hapaMbali na uzinduzi huo Naibu waziri huyo alipokea msaada wa madawati hamsini (50) yenye thamani ya Tsh. Millioni 5 kwa ajili ya shule ya sekondari Magao pamoja na vifaa kwa ajili ya kupaua (mbao zaidi ya 700 na Misumari) vyenye thamani ya Tsh. Milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Nganje, vyote hivyo ikiwa ni msaada toka benki ya NMB TanzaniaAkikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mtendaji mkuu wa Benki hiyo, Msimamizi wa Biashara za serikali na Mahusiano ya benki ya NMB Bi. Vicky Bishubo aliyeambatana na meneja wa benki hiyo wilaya ya Mkuranga Ndg. Joseph Iramba, alisema msaada huo ni kwa ajili ya kuendeleza nguvu zilizoanzishwa na wananchi wa kijiji hicho lakini pia ni utaratibu ambao benki hiyo imejiwekea kwa kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwa wananchiKwa upande wake naibu waziri huyo aliunga mkono jitihada za ujenzi wa zahanati kijijini hapo kwa kutoa mifuko hamsini ya saruji kwa kijiji hicho, ili kumalizia ujenzi wa kituo hicho cha AfyaWakiongea mara baada ya kupokea msaada huo wakazi wa Nganje walionesha kufurahia ujio wa kiongozi huyo wa serikali na kupongeza jitihada zilizofanywa na Diwani wa kata hiyo ambaye pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga Ndg. Juma Abeid kwa kushirikiana na Benki hiyo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.