Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya ameipongeza Asasi ya PWAMAO kwa kusaidiana na Serikali kufuatilia ubora wa huduma zinazotolewa na Maduka ya Dawa muhimu huku akiwahakikishia kuwanao bega kwa bega katika jitihada hizo hatmaye wananchi wapate huduma stahiki.
Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Filberto Sanga katika kongamano la Afya la wamiliki wa Maduka ya Dawa muhimu Wilayani Mkuranga, Muya ameitaka Asasi hiyo kuendelea kusimamia vema shughuli zao sambamba na kuongeza jitihada zaidi kuwatafuta wadau wengine waweze kuisaidia Wilaya katika changamoto mbali mbali zinazohusiana na Sekta ya Elimu
Akizungumza kwenye hafla ya kuwakabidhi watu wenye ulemavu wa miguu na macho baiskeli (10) na vifaa vya kusaidia kuona vilivyotolewa na Asasi hiyo jana, Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt Stephen Mwandambo aliwataka walengwa kutoka Kata kumi zilizobahatika kupata vifaa hivyo kuhakikisha wanavitunza vizuri ili viweze kuwasaidia kwa muda mtefu
Aidha Mwandambo alimpongeza Mwenyekiti wa Asasi ya wamiliki wa Maduka ya dawa muhimu Mkoa wa Pwani Salum Kipipa kwa kuandaa kongamano linalolenga kuwahimiza wamiliki hao kufuata kanuni na sheria za utoaji wa huduma hiyo ambayo inagusa kwa karibu maisha ya watu.
Pamoja na hayo Daktari huyo ametoa onyo kali na kuweka bayana kuanza msako mkali vitongoji vyote ili kuyabaini maduka feki ambayo hayajafuata utaratibu kuanzishwa kwake sambamba na wamiliki wote wanaofanya vipimo vya Afya ndani ya Maduka yao na kuahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Akitoa neno la shukrani Diwani wa Kata ya Mbezi Rashidi selungwi (ccm) alimpongeza Mdau Ahmed Salim ambaye hivi karibuni aliichangia Wilaya Sh. Milioni mbili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa Madawati sambamba na kuiwezesha Asasi ya Pwamao kwa kuwapatia vifaa hivyo huku akimhakikishia kuendelea kushirikiana nae katika kuleta Maendeleo Mkuranga.
Katika Mgao huo Hospitali ya Wilaya nayo imebahatika kupata Baiskeli (1) ambayo itatumika kuwabebea wagonjwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.