Taasisi ya Qamar Foundation iliyopo Nchini Canada imetoa msaada wa Maziwa aina ya “Lactogen 1” katoni mbili na nusu kwa ajili ya watoto wasio na wazazi kwa lengo la kuunga mkono mikakati mbali mbali ya kuboresha afya za watoto wa Wilaya Mkuranga.
Zoezi hilo limefanyika leo katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa Pwani ikiratibiwa na Afisa Lishe (W) Bi Vumilia Ngandambwa “ alisema anaishukuru sana na kuipongeza Taasisi ya Qamar kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha afya za watoto wanaokumbwa na changamoto mbali mbali zinaimarika kupitia misaada wanayoitoa”
Akizungumza katika makabidhiano hayo Bi Naima Mlawa mkazi wa kijiji cha Sotele kilichopo kata ya Dondo “ alisema anaishukuru sana taasisi ya ya Qamar Foundation lakini zaidi anawashukuru wauguzi na madaktari wa hospitali ya wilaya kwa kuwasaidia na kuwawezesha kuwapatia misaaada inayotolewa na wahisani kuja kwa walengwa na kuwezesha kuitumia pale inapobidi pasi na kuwa na ubadhilifu wa misaada hiyo kama ambavyo ingeweza kufanywa na wataalamu ambao sio waaminifu kwenye jamii wanayoihudumia
Aidha mnufaika huyo, aliongeza kwa kusema maziwa hayo yatawasaidia sana wajukuu zake ambao wamezaliwa Mapacha kwa kipindi ambacho mama wa watoto hao amepatwa na changamoto ya maradhi ya moyo ambayo imepelekea kuhamishwa na kwenda hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi..
Naye bi Salma Mihiko katibu wa idara ya afya na katibu wa kamati ndogo ya Maafa alisema anawashukuru sana viongozi wa taasisi ya QAMAR FOUNDATION na amewataka wafadhili wengine kujitokeza kwa wingi na kuweza kutoa misaada mbalimbali ambayo itawezesha kuimarisha afya za watoto wenye mahitaji ikiwemo vifaa tiba na lishe.
Katika kuhitimisha kwake bi Salma Mihiko amesema wamepokea barakoa mia moja (100) kwa ajili ya kuwagawia wagonjwa wanaokuja katika hospitali ya wilaya kwa lengo la kupiga vita dhidi ya ugonjwa wa Covid19 unaosababishwa na kirusi cha corona…
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.