Halmashauri za wilaya na miji Mkoani pwani wametakiwa kushirikiana kwa karibu na wakala wa misitu nchini (TFS) wa maeneo yao ili kutokomeza ukataji miti, kuchoma mkaa , na upasuaji mbaoili kuepusha upungufu wa moto wa asili unaoshamiri kwa kasi kubwa.
Akizungumza na wananchi wa Mkoani humo kweye siku ya upandaji miti kitaifa ambayo kimkoa imefanyika kitongoji cha kamegere kata ya vikindu wilayani Mkuranga , Mkuu wa mkoa Mhandisi Evarist Ndikilo alipongeza wilaya hiyo kukubali uenyeji na kufanikisha zoezi zima la kupanda miti.
Mhandisi Ndikilo aliyewakilishwa na mkuu wa wilaya ya Mkuranga Ndugu Filliberto Sanga aliwataka wananchi kuongeza juhudi ya kupanda miti ambayo ni hazina iliyotukuka kwa matumizi mbali mbali kiuchumi,uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji.
Aidha alitaja athari zingine kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanachangia kuongezeka kwa joto juu ya uso wa dunia linalochangia kuyeyuka kwa barafu na kuongeza kina cha maji ya bahari hatimaye kumezwa baadhi ya visiwa.
Awali afisa misitu mkoa wa pwani Pierre Ndyamagwa alisema misitu iliyopo kwenye maeneo ya makazi ya watu inakatwa hovyo kutokana na maeneo hayo kutomilikiwa kisheria
Afisa huyo alizitaka serikali za vijiji kutokuuza ardhi kwenye maeneo yenye misitu hata kama hayajahifadhiwa kisheria, huku akiagiza wakala wa misitu nchini (TFS) wilaya zote kutuma pesa zinazolipwa na wafanyabiashara wa mazao ya misitu kwenye Halmashauri husika ili kuwahi maandalizi ya upandaji miti.
Akishukuru kaimu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Shabani Manda alimhakikishia mgeni rasmi watalinda kwa nguvu zote misitu huku akiahidi kuwasimamia watendaji vijiji watekeleze maagizo ya MKOA.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.