Wakala wa usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Imeendesha mafunzo maalumu ya usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka mitano (5) kwa watendaji wa kata na wawakilishi kutoka vituo vinavyotoa huduma ya mama na mtoto wilayani Mkuranga Lengo ikiwa ni kutoa vyeti bure kwa watoto wote walio na umri chini ya miaka mitano
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya, Dkt. Steven Mwandambo aliwataka walengwa wa mafunzo hayo (Wasajili) kuzingatia weledi katika utoaji wa vyeti hivyo ikiwamo kuzingatia usahihi wa taarifa za wazazi na watoto kwani vyeti hivyo ni haki ya kila raia lakini kutokuwa makini kunaweza kupelekea kusajiliwa kwa watu wasio na sifa mathalani watu wasio Raia wa Tanzania.
Aidha Afisa Usaili kutoka RITA, Bi.Emmanuela Mwingira akiongea na ’Mkuranga DC’ alisema wameamua kufikia hatua hiyo ili kupandisha asilimia ya usajili wa watoto kutoka 13% ilivyo sasa hali inayoigharimu serikali kushindwa kupata taarifa sahihi za vizazi na vifo
Aliongeza kuwa, raia wengi wanashindwa kujisajili kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo umbali na gharama, Hivyo mara baada ya mafunzo hayo raia wataweza kupatiwa vyeti hivyo bure katika ofisi za kata ama Zahanati za vijiji vyao husika tofauti na ilivyokua awali kulazimu kila muhitaji kwenda kufuata vyeti hivyo katika ofisi za wilaya pekee.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Mkuranga Bi. Phoibe Samuel Peter akielezea umuhimu wa zoezi hilo lenye kauli mbiu “Mtoto anastahili cheti cha Kuzaliwa mpe Haki yake” alisema, kuwa cheti ni faida kwa mtoto kwani ndio utambulisho wake wa kwanza hivyo ni haki yake na pia itamuwezesha mtoto kupata elimu na maisha bora
Jumla ya washiriki 169 wanapatiwa mafunzo hayo yaliendeshwa na RITA kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na Canadian International Development Agency (CIDA) na yatadumu kwa siku tatu
Afisa Ustawi wa jamii Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Phoibe Samuel Peter akitoa mada wakati wa semina hiyo
Washiriki wakikabidhiwa vitendea kazi / simu za lununu zitakazotumika kusajili vyeti hivyo
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Eng: Mshamu Munde akitoa hutuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya Steven Mwandambo na kushoto ni Afisa usajili toka RITA Bi. Emmanuela Mwingira
Washiriki wakila kiapo ikiwa ni ishara ya kutenda haki na weledi katika utendaji wao
Wawezeshaji wa semina wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.