Afisa Mwandikishaji (RO) Wilaya ya Mkuranga Patric Saduka ametoa wito kwa waandikishaji wasaidizi na waendeshaji wa vifaa vya Bayometriki kuhakikisha wanavitumia vifaa vyote vitakavyotumika katika uboreshaji pamoja na kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume.
Wito huo ameutoa tarehe 14 Mei 2025 wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili katika ukumbi wa Shule ya msingi Perfect Destiny.
Saduka amesema ni muhimu kuwepo na ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji pamoja na Serikali, Vyama vya Siasa na wadau wengine wa Uchaguzi.
Aidha amewataka kuwa na ushirikiano mzuri na wa karibu na wataalam wa Tume ya Uchaguzi wakati wote pindi wanapohitaji ufafanuzi au maelekezo katika kutekeleza majukumu yao.
Awali Saduka amesema Mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kwa lengo la kuleta uwazi katika zoezi hilo lakini pia watatumika kuwatambua wapiga kura wa eneo husika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.