• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
    • TASKSMIS |
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Rasimali watu na Utawala
      • Industrial, Trade and Investment
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Mipango,Sera na Takwimu
      • Ardhi na Maliasilli
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Uongozi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Sera
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Photo Galley
    • Habari Mpya
    • Matukio

Salfa ya wizi yapatikana Mkuranga

Posted on: September 4th, 2017


Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imekamata salfa ya wizi mifuko 247 yenye thamani ya Tshs 6,916,000 ambayo  katika kijiji cha Msonga ikiwa katika maandalizi ya kuanza kuuzwa.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh.Filberto Sanga akizungumza leo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya pamoja na baadhi ya watendaji na wataalamu mbalimbali alisema”Siku ya alhamisi ya tarehe 3/08/2017 usiku  walibaini kuna salfa nyumbani kwa mtu hivyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi salfa hizo zilikamatwa na

kuhifadhiwa zikisubiri upelelezi ukamilike”.

Mh Sanga alisema kuwa baada ya upelelezi kukamilika salfa hizo zitagawiwa kwa wananchi wa Mkuranga kama salfa za awali zilivyogawiwa.

Adha Mh Sanga ametoa wito kwa watendaji wote wa serikali kuwa waaminifu na kuacha ubadhilifu na udanganyifu katika mali za umma.

Mh Sanga alisema Wilaya ya  Mkuranga ilipokea pembejeo za ruzuku kwa asilimia mia moja ya korosho kiasi cha kilo 453,875 sawa na mifuko 18,155, salfa ya unga katika awamu 4,yaani mifuko 8,314,mifuko 5,998,Mifuko 2,390 na Mifuko 1200. Pia jumla ya lita 6,886 za salfa ya maji, lita 1,231 dawa za wadudu  na mabomba 41.

Kupitia kamati ya Pembejeo ya Wilaya mgao wa pembejeo hizo ulifanyika kwa kila kijiji kwa kutumia kigezo cha idadi ya mikorosho.

Mh Sanga alisema pamoja na mafanikio ya ugawaji wa pembejeo hizo kuna changamoto zilizojotokeza ikiwemo udanganyifu kwa upande wa wakulima kwa kutoa takwimu za uongo juu ya idadi ya mikorosho waliyonayo kwa lengo la kupatiwa mgao mkubwa wa pembejeo. Vilevile pembejeo kutotosheleza mahitaji halisi kwa wakulima kwani kuna upungufu wa takribani tani 346 za salfa ya unga, lita 7,000 za salfa ya maji, lita 3,000 za dawa za wadudu na mabomba 85. Pia changamoto kwa baadhi ya watendaji wa vijiji kutowasilisha takwimu za mikorosho kwa vijiji vyao mfano kijiji cha Marogoro kata ya Vianzi na kusababisha wakulima wa maeneo hayo kukosa pembejeo.

Akizungumza namna ya kutatua changamoto hizo Mh sanga alisema mpaka sasa Wilaya imepeleka maombi ya kupatiwa nyongeza ya pembejeo na imefanikiwa kupatiwa tani 10 zaidi ya salfa ya unga lakini pia watendaji wameelimishwa juu ya ukusanyaji wa takwimu sahihi za mikorosho kutoka kwa wakulima japo takwimu hizi hazikuweza kutumika tena msimu huu bali zitatumika kwa msimu ujao.

Mh Sanga alisema wakulima wengi wamehamasika kusafisha mashamba yao hasa baada ya kuambiwa kigezo kimojawapo cha kupatiwa pembejeo ni kuwa na shamba la mikorosho lililopaliliwa, vilevile  Wilaya imeweza kupata takwimu za awali za idadi ya mikorosho waliyonayo wakulima.Hii itasaidia kutathmini mahitaji halisi ya pembejeo.

Julita Bulali Afisa kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Mkuranga alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa takwimu sahihi kutokana na wakulima kutokuwa na ushirikiano, hivyo katika harakati za kupambana na changamoto hiyo viongozi wa vijiji wakiwemo wenyeviti wa vitongoji wameagizwa kubainisha idadi ya  mikorosho.

Wilaya ya Mkuranga ni miongoni mwa Wilaya zinazolima korosho na kwa Mkoa wa Pwani inaongoza kwa kuwa na takribani mikorosho milioni tatu na inazalisha  wastani wa tani 9,000 kwa mwaka.

Katika msimu wa 2016/2017 wilaya imeuza korosho kiasi cha kilo 6,647,081 na kuingiza jumla ya Tshs 15,846,498,022.


Matangazo

  • TANGAZO LA VITUO VYA USAILI January 21, 2025
  • ORODHA YA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA January 21, 2025
  • Tazama vyote

Habari Mpya

  • MADIWANI MKURANGA WAPITISHA TAARIFA YA MAENDELEO ROBO YA TATU

    April 29, 2025
  • KIJANA WA MLENGWA WA TASAF ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

    March 03, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA IMEFANYA UZINDUZI WA MIRADI YA (TI)

    March 01, 2025
  • WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA

    February 10, 2025
  • Tazama vyote

Video

SIMAMIENI MAADILI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya Ruhusa ya Ugonjwa kwa Watumishi (Sick Sheet Form)
  • FFARS user manual
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2020
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • uchaguzi wa wanafunzi kujiunga kidato cha kwanza 2020/2021 Mkuranga
  • Barua pepe za ofisi za watumishi
  • Fomu ya Likizo kwa Watumishi
  • Fomu ya Ruhusa kwa Watumishi
  • Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara

Tovuti Linganifu

  • TAMISEMI
  • e-GA
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Ajira
  • Ikulu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Baraza la Mitihani la Tanzania
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
  • Mkuranga Tasks Management Information System (Tasks MIS)

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

    Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania

    Telephone: +255232110038

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.