SERIKALI kupitia Bodi ya Korosho Tanzania imejipanga kuhakikisha pembejeo za korosho kwa`msimu ujao wa`mwaka 2017/18 kwa wakulima wa zao la korosho zinawafikia wakuima kwa`wakati kwani mpaka sasa tani 2,890 za Salfa ya unga na lita 30,000 za viatilifu vya maji zimeshawasili katika Bandari ya Dar es Slalaam.
Akifungua mafunzo ya ya kilimo bora na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wakulima na wapuliziaji dawa wa Mkoa wa Pwani,Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbeto Sanga alisema lengo la mafunzo hayo ni kutoa nafasi ya kuwafunza wawakilishi wa wakulima na wadau wa zao la korosho namna ya kuhudumia zao hilo.
Alisema katika msimu uliopita wa mwaka 2016/17 upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho ulikuwa wa kuridhisha kutokana na kupatikana kwa fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi kwa wakati kulikowezesha uagizaji wa pembejeo nao ufanyike kwa wakati.
“Kupatikana kwa fedha za ushuru wa mauzo y korosho nje ya nchi kwa wakati kuliwezesha uagizaji wa pembejeo ufanyike kwa wakati muafaka na hivyo kumfikia mkulima kabla ya muda wa kupuliza dawa kwenye mikorosho haujfika,”alisema Sanga.
Aliongeza kuwa, kiasi cha pembejeo kilichoagizwa kilikuwa cha kuridhisha mpaka sasa bado vipo viuatilifu vilivyobaki katika maghala ya Mwendapole Kibaha na Naliendele Mtwara pamoja na Mtwara sambamba na Mtwara mjini.
Alisema katika msimu wa`mwaka 2017/18 serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania inejipanga vizuri kuhakikisha kuwa pembejeo za korosho zinawafikia wakulima kwa wakati kwani mpaka sasa tani 2,890 za salfa yaunga na lita 30,000 za viuatilifu vya maji zimeishawasili katika bandari ya Dar es Salaam na ziko katika hatua ya kusafirishwa katika vituo vilivyotengwa katika Halmashauri zote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania ambaye ni Mwenyekiti tawi la Dar es Salaam Mangile Malegesi ambao ndiyo waandaaji wa mafunzo hayo alisema mbegu zilizowasili zinatarajiwa kuanza kutolewa mwezi ujao.
Aidha aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri kwa wengine kwa kuzigatia kuwa zao hilo ni kiini cha uchumi.
Hata hivyo alisema mafunzo haya yamelenga kuifikia mikoa yote inayojishughuisha na zao hiloambapo awamu ya kwanza elimu juu ya utunzaji sahihi za zao hilo umeanza kufanyika kwa wakulima na wadau wa zao hilo wa mikoa ya Pwani naTanga ambapo awamu ya pili itakuwa ni kwa mikoa ya Mtwara, Lindi,na Ruvuma.
Mwisho.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.