Serikali imetenga shilingi Bilioni 37 kwa ajili ya utekelezaji Mradi wa ujenzi na usambazaji wa miundo mbinu ya umeme katika vijiji vyote Vilivyopo ndani ya Mkoa wa Pwani
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati Steven Dejauka Byabato Agosti 26,mwaka huu wakati akizindua utekelezaji wa Miradi ya umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili katika Kijiji cha Mikele kata ya Njia Nne Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Amesema kwa kutambua mahitaji ya umeme nchini serikali inatarajia kutekeleza miradi ya umeme katika vijiji mbalimbali nchini na kwamba ikiwamo mradi wa umeme unaotelekezwa katika vijiji vya Mikele Kata ya njia nne wilaya ya Mkuranga.
“Serikali imetenga Shilingi Bilioni 37 ambazo zinakwenda kutekeleza miradi ya kusambaza umeme katika mkoa wa Pwani na Wilaya ya Mkuranga imetoa shilingi Bilioni 11 na kati ya hizo shilingi milioni 664 zinaenda kutekeleza mradi wa kusambaza umeme katika Kata ya Njia Nne na shilingi milioni 82 itatumika katika Kijiji cha mikele.’Alisema
Aidha akikagua miradi hiyo Byabato alitoa agizo kwa wasimamizi wanaotekeleza wa miradi ya kusambaza umeme kuhakikisha wanatoa kipaumbele katika maeneo ya Umma ikiwemo Shule, hospital, zahanati, na nyumba za ibada
Mkuu Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri Ally aliishukuru serikali kwa kufanisha utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme katika wilaya yake na ameahidi kuwasimamia wakandarasi waliopewa zabuni za kutekeleza miradi hiyo
Khadija amesema kama Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga hatakuwa tayari kuona miradi inachelewesha bila sababu yeyote ya msingi na hivyo kusababisha ucheleleweshaji wa azima ya serikali inayotaka kila Kijiji kipate umeme
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah Ulega akatumia fursa hiyo kumuomba Waziri Byabato kusaidia kuharakishwa suala la uwashaji wa umeme katika Kijiji cha cha ming’ombe
“Mheshimwa Naibu Waziri wa nishati sisi tutafarijika sana iwapo tukiona maeneo ya mikele, miteza, na ming’ombe yanawaka umeme ndio waendelee kwenda kuwasha umeme katika vijiji vingine vilivyopo wilaya ya Mkuranga.Alisema Abdalah Ulega.
Diwani wa njia nne amemuhakikishia mh Naibu waziri kuzungumza na wananchi wa kata hiyo kukubali kutoa maeneo ya kupitisha umeme bila kudai fidia isipokua wameomba kusaidiwa ujenzi wa barabara inayotoka mwarusembe hadi mikele
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.