Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Filberto Sanga amewataka wananchi wanaoishi katika eneo linalozunguka msitu wa vikindu kusitisha kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo utalii, uvuvi na uwindaji katika Msitu huo hii ni kutokana na taharuki iliyotokea kwa kudhaniwa kuwa na Simba katika eneo hilo la hifadhi
Akizungumza katika viunga vya Msitu huo jana mara baada ya kuwasili kwa lengo la kuambatana na askari wa wanyamapori katika dolia ya kuwasaka simba hao Sanga alisema tayari shughuli za kuwatafuta Simba zimeshaanza hivyo anawataka wananchi wote kusitisha shughuli zote ambazo ameziainisha.
Aidha sanga alisisitiza kwa kusema wakati uliopo ni wa kuwatafuta simba ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea kutokana na uwepo wa wanyama hao na hakuna mda wa kushughulikia vitu vingine katika eneo hilo hivyo shughuli zote zisimame mara moja.
Mkuu wa Wilaya alisema simba hao wameanza kutajwa katika Wilaya kuanzia jumatatu katika maeneo ya kisiju Pwani kisha kinamama walikwenda kuchita maji mtoni maeneo ya utunge kata ya mwandege na vijana wengine huko kipala mpakani waliwaona walipoenda kutafuta Kamba.
Yohana awise ni miongoni mwa wananchi waliowaona Simba hao Jike na Dume wakati walipokua wanavua samaki katika mto Mkangaza ambao upo katika msitu huo wa Vikindu. Yohana aliongezea kwa kusema anaiomba serikali kuharakisha kuondoa simba hao haraka ili kupunguza taharuki kwa wananchi wanaoishi karibu na eneo la msitu na hata wale wanaokuja katika eneo hilo kwa lengo la kufanya utalii na shughuli zote za kibinadamu.
Naye Bi. Zawadi Malunda Mdhibiti na Mhifadhi wa wanyama pori, wanyama wakali na waharibifu (TAWA) alisema tayari wapo katika eneo la tukio na tayari wameshaanza juhudi za kuwasaka simba hao, ambapo ameahidi kutoondoka katika msitu huo hadi watakapofanikiwa kuwapata simba hao.
Malunda alimalizia kwa kusema anaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa kila wanapobaini mnyama yoyote wa tofauti katika maeneo yao ili kufanikisha upatikanaji wa haraka wa Simba hao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.