Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imeadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika katika viwanja vya shule ya Msingi Dundani katika kijiji cha Dundani Kata ya Mkuranga.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali ambae ndio mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo amesema mtoto ana haki ya kupata Elimu bora, Afya bora, Chakula bora,Malazi pamoja na makazi mazuri endapo tutahakikisha mtoto anapata yote hayo basi tutaweza kujenga Taifa lenye watoto bora ambao wataweza kutimiza malengo yao ya baadae.
Aidha amewataka wazazi kuwalinda watoto dhidi ya watu ambao wanawafanyia vitendo viovu na kuwasihi wazazi kutoa taarifa katika vyombo husika endapo wanapobaini mtoto kafanyiwa kitendo kiovu hata kama aliehusika ni mwanafamilia basi anatakiwa kuripotiwa na sio kuyamaliza kifamilia.
Pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuweka elimu bure kwa kidato cha tano na cha sita na kuwataka wazazi kuhakikisha watoto wanafaulu vizuri na kuwapeleka katika shule walizopangiwa bila shida na hofu yoyote.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja amewashukuru wanafunzi pamoja na wazazi waliokuja kwenye Maadhimisho hayo na kuwataka wazazi hao kuwapa watoto malezi bora ili waje kuwa viongozi bora hapo baadae.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.