Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mh. Khadija Nasri Ali leo Agosti 29,2022 amefanya kikao na wajumbe wa kamati ya huduma ya Afya ya msingi kwa lengo la kupanga mikakati ya namna ya kuendesha zoezi la Chanjo ya Polio linalotarajiwa kuanza mapema Septemba
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi Mh. Khadija amemtaka katibu wa chanjo wilaya Dkt. Ali Mbikilwa kusimamia zoezi kwa weledi ili kuleta matokeo chanya kwa kuhakikisha kila mtoto mwenye Umri chini ya miaka Mitano anapatiwa chanjo ya Polio.
Aidha Mh Nasri amewata wataalamu kutumia nafasi zao kukanusha upotoshaji wowote unaoweza kutokea kwa lengo la kukwamisha zoezi la chanjo lisifanyike kwa ufanisi.
Akipokea maelekezo hayo Mganga Mkuu wa Wilaya Ali Mbikilwa amemuahidi Mkuu wa wilaya kutekeleza jukumu hilo pasi na kuwa na dosari yoyote
“ nikuahidi Mh. Mkuu wa wilaya mimi sambamba na wataalam wenzangu wa afya tunaenda kulifanya zoezi hili la utoaji wa chanjo na kwa namna tulivyojipanga na kuhakikishia kuyafikia malengo tuliyojipangia na zaid ya vile tutarajiavyo” alisema.
Naye Mwenyekiti kwa huduma za jamii na Diwani wa Kata ya Mkamba Mh. Hassan Dunda alisisitiza wataalamu wa afya waendeshe zoezi hili kwa kuwatumia wenyeviti wa Vijiji kwa kuwapelekea nyumba kwa nyumba kwa kuwa wao ndio wenyeji wa eneo hilo na wanajua nyumba gani ina mlemgwa wa chanjo hiyo.
Zoezi la chanjo ya Polio kitaifa linatarajiwa kuanza Septemba 1-4, 2022.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.