Mkuu wa Dawati la kuzuia Rushwa ( Utafiti na udhibiti ) Takukuru Wilaya ya Mkuranga Hafsa Kitime, amewataka wakuu wa Idara pamoja na wakuu wa vitengo kushirikisha wahandisi wa ujenzi katika miradi mbalimbali vijijini na kuepuka kupitisha malipo ya mafundi bila kupata ushauri kutoka kwa mhandisi wa ujenzi.
Ameyasema hayo leo katika warsha iliyofanyika katika viwanja vya Godown Mkuranga na kuwasisitiza kufanya hivyo kutaondoa ubadhilifu katika majengo ya serikali na kuondoa mianya ya rushwa kwa watendaji wa Serikali.
Kitime amesema lengo la warsha hiyo ni kujadili kwa pamoja ili kuweza kuziba mianya ya Rushwa katika mfumo wa manunuzi ya umma kwa watendaji katika Wilaya ya Mkuranga.
Naye Mkuu wa Dawati la uchunguzi (TAKUKURU) wilaya ya Mkuranga Beneti Kapinga, amesema wameamua kuandaa warsha hiyo kutokana na ofisi ya Takukuru Wilayani Mkuranga kupokea 19% ya malalamiko ambayo mengi yameonekana katika sekta za Afya, Elimu Msingi na Sekondari pamoja na vijijini ambapo kumeonekana kuna changamoto nyingi katika mifumo ya manunuzi.
Akihairisha warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, afisa manunuzi wilaya ya Mkuranga Omari Mshamu amewataka wadau wa manunuzi kuisoma sheria ya manunuzi ili kuondoa matatizo katika kufanya manunuzi ya miradi ya serikali.
Warsha hiyo iliyowajumuisha wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri hiyo pamoja na walimu wakuu na kamati zao, watendaji wa vijiji na wadau wengine wamekubaliana ndani ya miezi mitatu kutakuwa na ufuatiliaji wa maazimio ya warsha hiyo ambapo kubwa ni kila mmoja afuate sheria na taratibu za manunuzi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.