Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga Mkoa wa Pwani wametakiwa kuhakikisha wanamsaidia Raisi Dkt, John Pombe Magufuli , kuikagua miradi ya ya maendeleo maeneo yote kuanzia kwenye Vitongoji iwe na ubora
Akitoa elimu kwa viongozi hao wa kamati za maendeleo kata kwenye Hoteli ya Flex jana kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Wilayani humo, Ismail Bukuku aliweka bayana majukumu yao ni pamoja nakusimamia gharama ziendane na ubora wakeb
Aidha kiongozi huyo ambaye pia mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya aliendelea kuwashauri kuwa kwenye miradi yote wahakikishe yapo mabango yenye vielelezo vyote
Kwa upande wake afisa wa (TAKUKURU) anayeshughulikia dawati la elimu kwa umma Christina Kambwa aliwaeleza Madiwani hao kuwa miradi mikubwa inayosimamiwa na serikali kuu wafatilie kama upo wizi wowote watoe taarifa ngazi mbali mbali sambamba na ofisi yao
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.