Halmashauri ya Wilaya Mkuranga Mkoa wa Pwani imepewa ridhaa na ofisi ya Raisi (TAMISEMI) itenge bajeti ya kutengeneza barabara hatimaye mawasiliano yafunguke kwenye vitongoji na vijiji
Akizungumza na madiwan,i wataalamu ,na watendaji baada ya kukagua ukarabati wa wodi ya wazazi Hospital ya Wilaya mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa (TAMISEMI) Joseph Nyamhanga pamoja na kufurahishwa na ukusanyaji wa mapato aliwaagiza viongozi wa Halmashauri Mkuranga kutengeneza barabara zao wakati huu ambao bajeti ya wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) ni ndogo
Aidha Nyamhanga alikubaliana na mawazo ya kuanza upya ujenzi wa Hospitali hiyo kwa mpangilio mzuri huku akiahidi kuwaongezea pesa kadri bajeti itakavyoruhusu hatimaye wananchi waboreke kiafya na kuweza kuchangia maendeleo
Akizungumza matengenezo ya barabara kutoka Mkuranga mjini kwenda Kisiju katibu huyo aliwahakikishia wananchi itakamilika kwa awamu kama ilani ya uchaguzi (CCM) inavyobainisha kiongozi huyo alitumia fursa hiyo kuwaagiza waganga Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuwa ukarabati ,ujenzi na upanuzi unaoendelea kote Nchini kwa Zahanati na vituo vya afya wahakikishe unaendana na utoaji huduma bora kwa wagonjwa
Akimkaribisha katibu mkuu ,Mkuu wa Wilaya FILBERTO SANGA alimhakikishia kutokana na mahusiano mazuri ofisi yake ,madiwani, chama tawala (CCm) na wataalamu wa halmashauri yatafanikisha kikamilifu maagizo yote
Naye mkurugenzi wa Halmashauri Mhandisi Mshamu Munde alisema wamejipanga katika kukusanya mapato huku akitaja hadi mwaka wa fedha ulioisha tayari wameingiza sh. Bilioni 6.3 hali itakayofanikisha kukamilika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi sekta mbalimbali
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.