Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi DR. Dorothy Gwajima amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kote Nchini kusimamia miradi ya TASAF kikamilifu na kuhakikisha katika vikao vyao vya Halmashauri vya kila mwezi kunakuwa na agenda ya TASAF.
DR.Dorothy ameyasema hayo katika mkutano maalum wa wananchi wa Kata ya Kiparang’anda Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na TASAF Wilayani Mkuranga.
DR. amewataka wananchi Wilayani Mkuranga kutoa taarifa kwa wakati mara yanapotokea mabadiliko ndani ya kaya inayonufaika na mradi huo ambao kwa kata ya Kiparang’anda imebahatika kupata mradi wa uhawilishaji fedha.
Aidha amewataka waratibu wa mradi TASAF kutumia utaratibu mzuri na unaofaa katika kuwaondoa wanufaika wa mradi ambao wanaonekana tayari wamejikwamua kimaisha badala ya kuwaondoa kimya kimya bila ya taarifa ambayo huleta mkanganyiko wa kuhakiki taarifa.
Amesema katika kuhakikisha miradi hii ya TASAF inasonga mbele sambamba na dhamira ya Rais DR John Pombe Magufuli ya kuwaondoa wananchi wake katika uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo mwaka 2025.
Awali baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mratibu wa TASAF Wilayani Mkuranga Safina, DR. Gwajima amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga sambamba na Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde kwa kuwapatia chakula cha lishe watoto wenye mahitaji maalum katika Hospital ya Wilaya Mkuranga .
Mradi wa TASAF Wilayani Mkuranga unatekelezwa katika vijiji 77 kati ya vijiji 125 na wanufaika wa mradi huu ni kaya 4584.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.