Programu ya stawishi maisha inayosimamiwa na serikali ya Tanzania kupitia TASAF kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo UNICEF imezinduliwa katika kijiji cha Mkiu Kata ya Nyamato Wilaya ya Mkuranga.
Program hii imezinduliwa October 29,2024 ikiwa na lengo la kuboresha lishe kwa watoto wenye umri kuanzia 0 - 5,mama wajawazito na mabinti balee kwa kuwapa elimu juu ya lishe bora kupitia vipindi vya redio.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ipo katika kutekeleza mpango wa majaribio wa mpango stawishi maisha kati ya Halmashauri 18 zilizochaguliwa na kupelekea kuunda vikundi 30 ambavyo vipo katika Kata 13 na Vijiji 19 na wana kikundi watapata nafasi ya kukutana mara moja kwa wiki kwa lengo la kusikiliza vipindi vya radio vyenye maudhui yanayolenga kuelimisha na kuhamasisha umuhimu wa kujali lishe bora kupitia redio walizopewa.
Bw.Shedrack Mziray Mkurugenzi Mtendaji TASAF amesema mradi huu ni sehemu ya mtandao wetu mpana wa kupunguza utapia mlo kwa Kaya zilizopo katika mradi wa TASAF.Kupitia mpango huu tutakwenda kukuza maendeleo ya rasilimali watu na kuziwezesha Kaya kujiweka huru kutoka katika mnyororo wa umaskini kwa kuzingatia elimu ya lishe bora watakayopatiwa.
Aidha amesema usambazaji wa redio zinazotumia nguvu ya jua (solar) zitahamasisha jamii kushiriki mijadala kuhusu mbinu za lishe bora pamoja na kuelimisha na kuburudisha vipindi vitakuwa kila wiki kwa kipindi cha miezi sita (6).
Nae Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga ambae pia ndio Katibu Tawala wa Wilaya ameishukuru TASAF na wadau wa Maendeleo UNICEF kwa mchango wao wa kipekee katika mpango huu wa lishe bora kwa Kaya zilizopo katika mpango wa TASAF.
"Nawasihi wanajimii wa Wilaya ya Mkuranga kushiriki kikamilifu katika mpango huu na tulete matokeo bora katika Kaya zetu tuhakikishe tunawekeza katika lishe bora ili kuepukana na udumavu kwani serikali imewekeza hivyo tunapaswa kuvipa thamani vitu ambavyo serikali vinawekeza juu yetu."
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.