Wakala wa Misitu (TFS) Wilaya ya Mkuranga wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wamechangia kiasi cha Shilingi Milioni moja na Laki tatu kwa vikundi vya usafirishaji mizigo katika Bandari ya Kisiju Wilayani humo kwa ajili ya kutatua changamoto ya kuzama majahazi kwenye Bandari ya Kisiju kunakosababishwa na Mikoko.
Akikagua eneo hilo kwa Boti juzi baada ya kilio cha wananchi hao ambao asilimia (90) huendesha maisha yao kupitia Bahari ya Hindi, Ulega aliyeongozana na kiongozi wa TFS Wilaya, Christina Ngalawa na Vikundi vya Kusafirisha Mizigo ya Bandalini hapo aliweka bayana kuota kwa Mikoko mipya na mchaga umepelekea boti kutoka Mafia kukwama na zingine kuzama hapo Kisiju na kupoteza Mizigo.
Katika fedha hizo Ulega alichangia Shilingi Milioni Moja na Meneja wa TFS aliahidi kuchangaia shilingi Laki tatu navyo vikundi vilikuwa vimekusanya shilingi laki nne ili kutoa Mikoko ambayo itawezesha boti kupita katika eneo hilo kwa urahisi wakati wa kuingia na kutoka bandarini hapo.
Nae Meneja wa TFS Wilaya ya Mkuranga Chrisina Ngalawa amemwambia Mbunge na ujumbe wote alioambatana nao kuwa kuota kwa mikoko hiyo pamoja na uwepo wa lundo la mchanga ndani ya pwani hiyo ni mabadiliko ya Tabia nchi ndiyo chanzo cha uoto huo wa asili na kuwapa maelekezo ya kuondoa mikoko kwa upana wa mita 40 ili kuwezesha boti na majahazi kupita kwa urahisi na kuzuia ajali zinazoendelea kutokea kila mara katika eneo hilo.
Akihitimisha , Naibu Waziri aliwahakikishia wananchi hao kuwa bandari hiyo haiwezi kufa kwani watu wa Mafia Kaskazini wanategemea sana kuitumia bandari hiyo kusafirisha Mizigo yao kirahisi kutokana na ukaribu uliopo ambapo ni tofauti na wakitumia bandari ya Nyamisati huku akiwapa pole sambamba na kuahidi kuwapa viroba vya unga cha kilo 25 kwa wahanga walioezuliwa na kubomolewa nyumba zao kwa upepo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.