Timu ya Uwezeshaji Mradi wa SHURE BORA Wilayani Mkuranga yakamilisha kufafanya Mikutano ya Uhamasishaji na uanzishwaji wa Madarasa ya UTAYARI kwa watoto wanaotarajia kuanza Darasa la Kwanza Mwakani.
Timu hiyo ilitembelea Madarasa ya UTAYARI ya Mfano katika Kijiji cha Vianzi Kitongoji cha Kihonda na Darasa lingine lililopo Kijiji cha Marogoro Kitongoji cha Sangatini mwanzoni mwa wiki na kupata fursa ya kuongea na wazazi wa wanafunzi hao ili waweze kuimarisha Madarsa hayo na yaweze kufanikisha watoto wao kuwa na uelewa mkubwa mara wanapoingia Darsa la Kwanza.
Afisa Elimu Msingi Bi. Jessy Mpangala amewaambia wazazi kuwa wajizatiti kusimamia mkakati huu ili uwe endelevu kwani baadae huenda Madarasa hayo yakafanikisha kupata Shule shikizi na baadae shule kamili,
“Lakini pia tukaona hii Programu ije huku Vianzi kama ilivyo Nyamato ambako shule mama na watoto waliko ni mbali na vianzi pia kuna hiyo hali, kwamba shule mama iliko na Jamii inavyotawanyika na kujenga kwa kasi ni mbali kufika katika shule mama, kwa hiyo tukaona vituo hivyo vya UTAYARI vianzishwe huku vianzi, hivyo basi ni vema vituo vya utayari vikaanzishwa vikawa shikizi na baadae vikasajiliwa na vikawa shule ilikamilika” Afisa Elimu Msingi alisema.
Aidha wazazi hao wameshauriwa kutenga maeneo makubwa ya kuanzishwa Madarasa hayo ili yaweze kufanikisha ujenzi wa shule iliyokamilika kwa siku za baadae.
“lakini vigezo na mashari kuzingatiwa kigezo cha kwanza katika lile eneo ambalo tumeliandaa kwa ajili ya Darasa la UTAYARI lazima tuwe na “Plani B” ya kutafuta eneo lingine la wazi kubwa ambalo linapatikana ndani ya eneo letu ambalo tunaona baadae tunataka kujenga shule” Afisa Elimu, Elimu Maaalum Bi. Hellen Benjamin Alisisitiza
Wilaya ya Mkuranga Mpango huu wa uanzishwa wa Madarasa ya Utayari unatekelezwa katika Kata mbili (2) kati ya Ishirini na Tano (25) zilizopo, ambazo ni Kata ya Nyamato na Kata ya Vianzi, ambapo kila Kata itakuwa na Madarasa mawili (2) ya Mfano na kufanya jumla ya Madarasa Manne (4) yanayotekelezwa ndani ya Wilaya ya Mkuranga hadi sasa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.