Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Abdallah Ulega (MB) amemuagiza katibu mkuu wa wizara ya Mifugo na uvuvi kuunda timu ya wataalam ambao watashughulikia mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika Mkoa wa Pwani.
Akizungumza mbele ya wananchi wa kijiji cha Kondo Mwelanzi kata ya Bupu Wilayani Mkuranga hapo jana kwa lengo la kuwapa pole na kuwatia faraja wananchi wa kijiji hicho ambacho walivamiwa na kupigwa na wafugaji jamii ya wamang’ati katika sikukuu ya Eid El Haji.
“katibu Mkuu wizara ya mifugo na uvuvi atengeneze timu ya wataalam waje mkuranga,kisarawe,,Rufiji na Kibiti kwa sababu ng’ombe wanaotusumbua leo wametokea Kisarawe hivyo upo uwezekano mkubwa wakifukuzwa Mkuranga watakimbilia Rufiji na Kibiti” Ulega alisema
Ulega aliongeza timu ya wataalam itakayoundwa itahusisha Wizara ya Mifugo,Misitu,Ardhi wakishirikiana kwa pamoja na wataalam wa Halmashauri ili wapate majibu ya kisayansi kufahamu mifugo hiyo imetoka wapi na itakwenda wapi na watafutiwe eneo gani ili wakae salama ili kuepusha kuvamia mashamba ya wakulima kila siku.
Ulega alisisitiza timu hiyo inatakiwa ije na suluhu ya kudumu kuhusu tatizo la wafugaji na wakulima.
“Nalaani kitendo kibaya kilichofanywa na wafugaji hao cha kujichukulia sheria mkononi,vyombo vya dola wahakikishe waliofanya jambo hili wanapatikana na sheria ichukue mkondo wake”.Ulega alisema
Aidha Ulega alisisitiza kwamba wananchi wanataka mifugo yenye tija lakini sio ufugaji wenye kuharibu mashamba na mazao ya wananchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mh Juma Abeid alitoa pole kwa wananchi waliopatwa na matatizo hayo na kuwataka jeshi la polisi kuhakikisha wamang’ati hao wanapatikana ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.