Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Hadija Nasri Ali amewataka wakulima kujitathmini kupitia maonesho ya nane nane ili kuweza kujiimarisha na kuanza kulima kwa kutumia nyenzo bora na za kisasa ili kuongeza uzalishaji.
Akizungumza na wakulima wa Mkuranga wanaoshiriki maonesho hayo kwenye viwanja vya J.K Nyerere Mjini Morogoro Mhe. Nasri alisema “Mkuranga ina ardhi nzuri kwa kilimo hivyo sisi tunaadhimisha sikuu hii ya nane nane tukijua kuwa inatugusa wengi na kugusa shughuli nyingi tunazozifanya hivyo tujipange kuitumia ardhi kwa ajili ya kufanya kilimo chenye tija.”
Aidha aliwataka kutumia mikopo ya kilimo inayotolewa kwa riba nafuu ambayo ikitumika vyema itawainua na kuwawezesha kuuza mazao mpaka nchi za nje.
Mh Nasri alimalizia kwa kuwakumbusha wananchi wa wilaya ya Mkuranga kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa ifikapo Agosti 23,2022.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.