Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Mh Abdallah Ulega amewataka wajasiriamali kubadilika kwa kufuga kuku na kuuza badala ya kusafirisha na kuuza mkaa maeneo mbalimbali ya Dar es salaam.
Waziri Huyo aliyasema hayo Leo hii wakati wa mafunzo kwenye jukwaa la wanawake wilayani Mkuranga lililofanyika katika ukumbi wa kiguza flex.
"Inawezekana tukiweka nia ya kweli tutafanikiwa tubadilishe kutoka kuuza mkaa kwenda kwenye matenga ya kuku" Ulega alisema
Ulega aliongeza kwamba lazima wakina mama wazalishe kuku wa kutosha na wafuge kibiashara ili kuwe na kuku wa kutosha kulisha viwanda vyote vya Mkuranga na Dar es salaam kwa ujumla.
Ulega alisema kuna mradi wa ufugaji wa kondoo unakuja hivi karibuni ambapo utaratibu wake utakuwa kopa kondoo lipa kondoo ikiwa na lengo la kuwasaidia wananchi kujikwamua kwenye umaskini.
Ulega alisisiza kwamba uongozi ni kuwasaidia wananchi watoke kwenye umaskini"Niko tayari kuwahudumia kwa nguvu na maarifa yangu yote ili mradi nihakikishe nawasaidia wananchi wangu kutoka hatua moja kwenye nyingine".
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Eng.Mshamu Munde alisema kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri imetenga Mil 433 kama asilimia kumi kutokana na mapato ya ndani ambapo asilimia 4 wanawake,4Vijana na 2 walemavu.
Munde aliongeza kwamba mikopo inayotolewa hawapewi watu ambao hawako tayari kufanya shughuli za maendeleo bali wale wenye utayari wa kufanya shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake wilayani Mkuranga bi Mariam Ulega ametoa pongezi kwa Viongozi wa Wilaya ya Mkuranga kwa kuwa bega kwa bega tangu kuanzishwa kwa jukwaa hili 2017.
Mafunzo ya ujasirimali kwa Jukwaa la wanawake wilayani Mkuranga yameanza rasmi Leo hii na kesho ndio yanamalizika yakiwa yameshirikisha wawakilishi kutoka Kata zote 25 za Mkuranga
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.