Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mhandisi Mshamu Munde amewapongeza viongozi wa sekta ya elimu msingi wa ngazi mbali mbali kwa mchango wao mkubwa katika kuboresha elimu.
Akizungumza katika hafla ya utoaji Tuzo kwa waliofanya vizuri Munde aliwaahidi kuwaboreshea maslahi yao na mazingira ya kufanya kazi ili kufanikisha malengo mahsusi ya Taifa kuelekea azma ya kufikia uchumi wa kati kabla ya mwaka (2025) huku akiweka bayana elimu ni mhimili mkubwa kufanikisha uwepo wa viwanda.
Akifungua hafla hiyo kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Ujenzi Mkuranga, Mwenyekiti wa kamati za kudumu huduma za Jamii Hassani Dunda aliipongeza sekta ya elimu chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde kwa kuboresha Miundo mbinu hali inayochangia kufanya vema kwenye mtihani wa Taifa uliopita na kufaulisha wananfunzi 7359 kati ya 8455 ambayo ni sawa na asilimia 86, huku Halmashauri ya Mkuranga ikiwa ni ya (5) Kimkoa.
Naye Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya Jessy Mpangala alitoa taarifa yake akiwapongeza Walimu pamoja na baadhi ya changamoto mbalimbali zinazowakabili bado wamefanya vizuri kwenye ufundishaji kiongozi huyo alisema,
“Halmashauri inaupungufu wa walimu (889) kwenye shule zote za msingi sambamba na miundombinu”.
Aidha Mpangala aliwageukia wazazi akiwataka kujenga utamaduni wa kufuatilia maendeleo ya taaluma kwa Watoto wao na kuacha kasumba ya kuwashawishi Watoto wafeli mitihani ili kukwepa kutembea umbali mrefu kufuata shule za sekondari.
Sherehe hizo zilipambwa kwa utoaji wa Tuzo mbali mbali zilizokabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ikiwemo utoaji wa vyeti na elfu (20) kwa mwanafunzi bora wa kike na wa kiume wa shule zote za serikali na binafsi zilizofanya vizuri.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.