Hali ya uelewa kwa jamii juu ya masuala ya ulaji sahihi imeongezeka ndani ya Wilaya ya Mkuranga ikilinganishwa na tathmini iliyofanyika kwa robo ya kwanza (Julai – Septemba 2018)
Hayo yamesemwa na Mratibu wa shughuli za lishe Wilaya Bi. Vumilia Ngandambo, wakati wa kikao cha kamati ya lishe Wilaya kwa robo ya pili, kilichofanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga.
Alisema, hali ya uelewa juu ya masuala ya lishe kwa makundi muhimu yaani watoto chini ya miaka mitano, wanawake walio katika umri wa kuzaa, vijana balehe na wazee imeongezeka ikiwa ni jitihada za Idara zote zinazotekeleza masuala ya lishe ambazo ni Elimu, Afya, Maendeleo ya jamii, Kilimo na Maji kupanga shughuli za lishe katika bajeti zao na kutekeleza mikakati iliyopangwa kwa wakati
“kwa mfano sasahivi tupo katika mchakato wa kuandaa bajeti ya 2019 / 20, kila mtu ameshajiandaa kutekeleza shughuli za lishe, lakini pia tumeona kwamba tathmini imekua nzuri sababu kila idara inaleta taarifa nini inafanya ndani ya ile robo, kwahiyo tunaona uelewa wa masuala ya lishe kuanzia watendaji wakuu umekua ni mzuri sababu Mkurugenzi na wakuu wa idara wanaelezea nini kimefanyika kwahiyo tunakwenda vizuri. Alisema, Bi. Vumilia
Aliongeza kuwa masuala mengine yalioratibiwa kutekelezwa katika robo ya pili ni pamoja kuzuia magonjwa yanayofanya jamii isipate virutubishi mwilini na lingine ni kuongeza uzalishaji wa chakula bora ili kusaidia jamii kupata chakula cha kutosha na kilicho bora
Wajumbe wa kamati ya lishe Wilaya wakifuatilia kwa makini dodoso la kikao hicho
Kwa upande mwingine, Bw. Gaidon Haule ambaye ni mdau wa kamati hiyo ya lishe toka shirika la JIMOWAKO, linalojishughulisha na masuala ya jamii hususani watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi alisema, kikao hicho kimesaidia sana kumtengenezea ‘network’ nzuri na wadau mbalimbali wa lishe na pia kupata takwimu na taarifa sahihi zitakazosaidia kupanga mikakati sahihi
Naye, Aniseth Bwakila ambaye ni mjumbe kamati hiyo alisema, mkazo zaidi utiliwe kuelimisha vijana juu ya masuala ya lishe kwani wao ndio kundi kubwa katika jamii na ndio watendaji wakuu kwasasa
Kikao hicho kililenga kutathmini shughuli za lishe zilizofanyika katika robo inayoanza Oktoba – Disemba ili kujua utekelezaji wa shughuli zilizopangwa kutekelezwa katika katika robo hiyo na vilevile kupanga mikakati ya robo inayofuta.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.