Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega ametoa kadi za bima ya afya kwa wazee 1000 ndani ya wilaya ya Mkuranga pamoja na vifaa mbalimbali kwa taasisi.
Hafla hiyo iliyofanyika tarehe 2 June 2025 katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga ilikuwa na lengo la kuboresha upatikanaji wa matibabu kwa wazee hao kwa urahisi
Ulega amesema kadi hizo za Bima za Afya kwa wazee hao zitaenda kuwanufaisha zaidi ya watu wanne (4) katika familia ambapo itaenda kupunguza adha kubwa ya gharama za matibabu katika familia hizo.
Pamoja na utoaji wa kadi hizo Ulega ametoa pikipiki 30 kwa viongozi wa Dini ambazo zitaenda kurahisisha utoaji wa huduma za kiimani katika shule pamoja na jamii, pia ametoa mashine ya kutolea nakala ( photocopy machine ) kwa shule za msingi na Sekondari kwa ajili kuhakikisha wanafunzi wanapewa mitihani ya kujipima mara kwa mara ili waweze kuwajenga katika masomo yao.
Aidha katika kuhakikisha huduma za afya zinatolewa vizuri Ulega ametoa majiko ya gesi 70 kwa Zahanati na vituo vya Afya vya serikali na binafsi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.