Katika kufunga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019, Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, jana alifanya Mkutano wa hadhara kwa wananchi wa jimbo hilo Lengo ikiwa ni kuelezea mafanikio ya kiutendaji kwa mwaka huu, kutoa dira ya mwaka unaokuja pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo.
Katika hadhara hiyo Mhe. Ulega alieleza mafanikio ya jimbo katika suala la miundo mbinu akitolea mfano ujenzi wa barabara ya Mkuranga – Kisiju, pamoja na madaraja katika maeneo korofi ikiwamo daraja la Kiembaemba, Huku akiahidi kuanza ujenzi wa barabara mpya katika maeneo ya Sangasanga, Nasibugani, Msanga nakadharika ili kurahisisha shughuli za usafirishaji.
Kwa upande wa Elimu alieleza kukamilika kwa ujenzi wa shule tatu mpya ndani ya mwaka 2018, ikiwamo shule ya Mlamleni, Miteza na Kipala
Mbali na yote hayo mbunge huyo pia alitoa lita 1000 za mafuta kwa ajili ya Greda la Halmashauri ili kurahisisha ukarabati wa barabara za mitaa ndani ya Halmashauri
Aidha alitoa shuka 100 zenye thamani ya Tsh. Mil 1 na laki 1 kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Mkwalia pamoja na vifaa vya Michezo kwa timu za Mpira wa miguu ndani ya wilaya hiyo
Baadhi ya vitu vya msaada villivyotolewa na Mbunge huyo kwa wananchi wa Mkuranga
Mara baada ya hadhara hiyo wananchi walioneshwa kufurahishwa na mkutano huo, ‘‘tunachotaka ni maendeleo Mkuranga na mbunge wetu anatuonesha mwanga, tuendelee kumuunga mkono ila atukumbuke na zahanati ya Kipera ina hali mbaya’’ alisema Juma Ndabwe mkazi wa Kipera Wilayani Mkuranga
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.