Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdallaha Ulega ametoa msaada wa vifaa vya shule wenye thamani ya shilingi Milioni 42,000,000 kwa wanafunzi wenye mazingira magumu na waliofaulu vizuri kidato cha nne pamoja na zawadi kwa walimu waliofaulisha Daraja la kwanza.
Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga ambapo ameweza kutoa mabegi ya shule, madaftari makubwa na madogo mashine ya kutolea nakala, vitu vingine ni rimu, Jezi za michezo, viatu na kiasi cha shilingi Laki 300,000 kama hamasa kwa walimu ambao shule zao zimepata Daraja la kwanza
Ulega amemshukuru Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utayari wake na kuthibitisha umuhimu wa elimu katika kuwakomboa watanzania kwenye elimu bure na sasa mpaka kidato cha tano na sita sambamba na kuongeza mikopo kwa wanaokwenda vyuo vikuu na sasa ametanua wigo mikopo inatolewa mpaka vyuo vya kati ili kuwafaa wasiokuwa na uwezo wa kusomesha Watoto ili wapate fursa ya kupata elimu.
Natoa zawadi hizi kama hamasa hasa kwa Watoto ambao wamefanya vizuri katika mitihani yao kwa kupata ufaulu wa Daraja la kwanza kidato cha nne kwani wametuheshimisha sisi wazazi wao sambamba na kuwapa misaada kwa Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwani wameshindwa kufika shuleni kwa kukosa vifaa vya kujisomea
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali amewapongeza walimu kwa jitihada kubwa wanayofanya ya kuweza kuhakikisha Watoto wanapata ufaulu mzuri Pamoja na hayo amewataka wazazi kuhakikisha wanasimamia vema maenfeleo ya Watoto wao shuleni na kuweka mahusiao mazuri na walimu kwa kushiriki vikao vya shule ambavyo vinatumika kujadili mustakabali wa Watoto hao
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.