Naibu WAziri wa Maji Meryprisca Mahundi ameupongeza ushirikiano mkubwa wa vi Viongozi Wilayani mkuranga Mkoa wa Pwani hali inayofanikisha utekelezajiwa miradi ya maendeleo.
Akizungumza baada ya kukagua chanzo cha maji na tenki kwenye kijiji cha mwanambaya leo Julai 27, 2021 kiongozi huyo alimtaka Mkandarasi Allain Makame kukamilisha kwa wakati huku akimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake Anthony Sanga kuhakikisha madeni ya mkandarasi anayafanyia kazi haraka.
Akiwa kwenye kisima cha Mkerezange Wilayani humo Naibu Waziri aliwahakikishia wananchi kuwa azma ya Rais Samia Suluhu kumtua ndoo mwanamke wanaitendea haki kwa kupeleka maji vijiji vyote Nchini.
Akiendelea aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuhakikisha wanaitunza miundo mbinu ili mradi ulete tija.
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo ya Mkamba ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu huduma za jamii Halmashauri ya Wilaya Hassan Dunda alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri wa Wizara hiyo Juma Aweso kwa mikakati yake usiku na mchana ambayo imezaa matunda kwa Wilaya ya Mkuranga kuondokana na kero ya kufuata maji safi na salama umbali mrefu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Hadija Ali alimuomba Naibu Waziri amfikishie salamu za shukrani kwa Rais kwa kuitendea haki Wilaya hiyo huku akimhakikishia kusimamia maagizo yake ikiwemo kusimamia uundaji wa Jumuiya za watumia maji ili makusanyo yaweze kutumika kwa marekebisho mbalimbali ya mradi huo.
Taarifa ya Kaimu Meneja wa Wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya Mkuranga Maria Malale ilitaja kijiji cha Kikundi kupelekewa maji baada ya miradi (3) kukamilika huku akihakikiha uzalendo wa Mkandarasii kufanya kazi kwa pesa yake wataulipa kwa kumtumia miradi mingine.
|
|
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.