Wilaya ya Mkuranga iliyopo katika Mkoa wa pwani inakabiliwa na tatizo la ugonjwa wa utapiamlo kutokana na kuwepo kwa lishe duni kwa baadhi ya wakazi wa Wilaya hiyo.
Mbali na lishe duni,pia imebainika kuwa ugonjwa wa UKIMWI umechangia kuwapo na ugonjwa huo kutokana na kuwapo wategemezi wengi katika familia.
Kuzalisha chakula kisichotosheleza mahitaji ya mwaka,hali duni ya uchumi ya jamii kutokana na kuwa na kipato kidogo.
Makundi ambayo yameathirika na utapiamlo katika wilaya ya Mkuranga ni kina mama wajawazito, na watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambao ukuaji wao ni wa shida.
Kaimu Mratibu wa Lishe Wilaya ya Mkuranga Bi Shani Tonga akiongea na Afisa Habari Mkuranga bi Boppe David wakati wa mahojiano katika ofisi ya Afya Wilaya alisema wagonjwa wa utapiamlo wilayani wanapatiwa tiba na lishe ya bure kwa wagonjwa wenye utapiamlo mkali.
“ushauri wa lishe unatolewa kwa wazazi, walezi na kwamba ushauri unahusisha unyonyeshaji wa mama kwa miezi sita.” Alisema
Anaongeza kuwa ulishaji wa watoto kuanzia miezi sita hadi 59 (miaka mitano kasoro mwezi mmoja) unaendana na kuwepo elimu ya lishe kwa wagonjwa hasa katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga.
Miongoni mwa mambo yanayofuatiliwa ni kuchunguza hali ya lishe kwa wagonjwa waliopo na ushauri katika masuala ya ulaji kwa motto aliye na umri chini ya miezi sita.
Bi Shani alisema kuwa jamii bado ina uelewa mdogo kuhusu maandalizi na ulaji katika jamii.kuongezeka kwa kasi ya ugonjwa wa UKIMWI inasababisha kuwapo wategemezi wengi katika familia na inapunguza uwepo wa akiba ya kutosha ya chakula kwani wazalishaji wanakuwa wamepungua.
Anaongeza kwamba Mkuranga ni miongoni mwa Wilaya zenye tatizo la utapiamlo, viashiria vyake vikiwa upungufu wa damu na waathirika wakubwa ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano, wajawazito na wanawake walio katika umri wa kuzaa.
Wengine ni wagonjwa wa muda mrefu, yatima, wazee na watoto waishio katika mazingira magumu.
Akizungumzia katika kipindi cha 2015 kuhusiana na utapiamo Shani alisema wagonjwa hospitalini kutokana na maradhi hayo walikuwa 3701 na kati yao 290 sawa na asilimia 7.8 walikuwa na viashiria vya upungufu wa damu.
Anaongeza kuwa kwa waliopata elimu ya lishe na unyonyeshaji walikuwa 1412 ni sawa na asilimia 39.1 na waliopewa rufani wako 319 ambao ni sawa na asilimia 8.9.
Mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mhandisi Mshamu Munde alisema kuwa mkakati wa wilaya ni kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa jamii ili kumaliza tatizo la upungufu wa damu katika wilaya ya Mkuranga.
Munde anaendelea kusema kwamba Halmashauri itaendelea kutenga bajeti ili kukidhi masuala ya lishe wilayani ikiwemo kuwa na walimu wa afya na wanafunzi watahusishwa kwa kuhamasishwa ulimaji wa bustani za mbogmboga na viazilishe.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.