Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Pwani Dkt Delphine Magere afanya ziara ya kujitambulisha kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga leo, hatua hiyo ya kujitambulisha ameifanya baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Bi Theresia Mbando aliyestaafu utumishi wa umma kisheria hivi karibuni .
Katika ziara hiyo Dkt Magere amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde kwa kutekeleza agizo la uchumi wa viwanda kwa weledi mkubwa ukilinganisha na wilaya nyingine alizotembelea “ umefanya vizuri sana katika kutekeleza agizo lakini najua peke yako usingefanikiwa bali kwa ushirikiano mlionao na wakuu wa Idara alisema”
Aidha katika uwasilishwaji wa hotuba yake Dkt Magere aliwataka watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa umma lakini pia alisisitiza kupewa ushirikiano ili wote kwa pamoja waweze kutimiza adhma ya kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Mkuranga pasipo vikwazo vyovyote.
Sanjari na hayo Katibu Tawala huyo alimtaka Mkurugenzi Mtendaji pamoja na wakuu wa idara kufanya tathmini ya kila sekta na matokeo ya tathmini hiyo yatumike kama fursa kwa wananchi wa Mkuranga katika lengo la kufikia uchumi wa kati, lakini pia alisisitiza wakuu wa idara kusimamia kwa weledi ukusanywaji wa mapato na kuzuia mianya ya rushwa ambayo kimsingi inarudisha nyuma maendeleo ya Nchi na jamii kwa ujumla…
Katika kuhitimisha kwake Dkt Magere alimtaka mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii kupata tathmini ya marejesho ya mikopo inayotolewa kwa walengwa ili waweze kujiridhisha na kuona kuwa kile kinachotolewa na Halmashauri kinafanya kazi na kurejeshwa ili wengine waweze kukopeshwa na kujiinua kiuchumi hatimaye maisha yao kuboreka
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.