Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) imezindua kampeni ya utoaji elimu juu ya yaliyomo ndani ya Ilani ya CCM kuanzia Mwaka 2025/2030.
Kampeni hiyo imezinduliwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa UWT, Zainab Khamis Shomari wakiwa katika ziara yao kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokuwa ikitekekezwa kutokana na ilani iliyopita.
Katika ziara hiyo Chatanda ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji na Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT wakiwa katika iijijini cha Mkamba Kata ya Mkamba Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani na kukagua miradi hiyo ya maendeleo.
Akizungumza na wananchi Chatanda amesema wao kama jumuiya ya wanawake CCM wamedhamiria kutoa elimu kwa wananchi hususani wanawake ili waweze kujua malengo na mipango ya chama hicho kwa wananchi wake.
“Tunajambo kubwa ambalo tunakusudia kulifanya hapa la uzinduzi wa utoaji wa elimu ya ilani upya ambayo itaanza kutekelezwa kuanzia 2025/2030 sisi kama UWT tumeamua kupita kuelimisha wanawake wenzetu na wananchi juu ya Ilani ambayo tumeizindua,” amesema Chatanda.
Chatanda na wajumbe hao wametembelea miradi 39 ya maendeleo katika wilaya hiyo ambayoimegharuimu zaidi ya Sh bilioni 200 katika utekelezaji wake.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.