Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga inawatafuta watoto ambao hawakupatiwa au kukamilisha chanjo kwa kipindi cha januari mpaka machi 2017,hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde wakati wa uzinduzi wa chanjo iliyofanyika kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga leo.
Mratibu wa Chanjo bi Anna Liachema aliendelea kusema kwamba Wilaya ya Mkuranga inaungana na Wilaya nyingine nchini kuadhimisha wiki ya chanjo duniani kuanzia tarehe 24-30/04/2017 ambapo walengwa wakuu kwenye zoezi la chanjo ni watoto walio na umri chini ya miaka mitano ambao hawajapata au kukamilisha chanjo.
Mratibu wa Chanjo aliendelea kufafanua kwamba kwa kipindi cha januari mpaka machi walilenga kuwapatia chanjo watoto 1761 lakini kuna baadhi ya watoto hawakupatiwa chanjo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kusafiri na kusababisha watoto 162 kutopatiwa chanjo.
Kaimu Mganga Mkuu Wilaya Dr Philemon Kalugira alisema kwamba wamejipanga vizuri kuhakikisha kwamba watoto ambao hawakupata chanjo wanatafutwa na kupatiwa kwa kufanya usimamizi wa karibu kwenye maeneo yenye watoto wengi.
Madhumuni ya wiki ya chanjo yamelenga kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo katika kukinga magonjwa na kuepusha vifo vya watoto vitokanavyo na magonjwa yanayozuilika,pia kuhimiza familia kupeleka watoto wanao stahili kupata chanjo ama kukamilisha ratiba ya chanjo katika vituo vinavyotoa chanjo.
Chanjo zitatolewa kwenye vituo 42 vinavyotoa chanjo,pia mobile 42 na outreach 25(huduma za mkoba)zitaendelea kufanyika katika maeneo yanayoangukia tarehe za wiki ya chanjo kama ilivyopangwa na kituo husika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.