Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Hassan Suluhu,amesema kuwa vijana wakipatiwa elimu ya stadi za maisha watafanikiwa kupata kazi nzuri viwandani na kama hawatakuwa na elimu wataishia kuwa vibarua katika viwanda.
Suluhu aliyasema hayo jana Mkuranga,katika ziara yake ya kutembelea Wilaya za Mkoa wa Pwani.
Samia akiwa katika kiwanda cha Gypsum cha Kisemvule,kilichopo Mkuranga alisema ili vijana waache kuwa vibarua katika viwanda wanatakiwa kusoma elimu ya stadi za maisha.
" Viwanda vinaanzishwa kwa wingi hapa nchini,kinachotakiwa ni vijana kusoma stadi za maisha ambazo zitawasaidia kupata ajira na kuachana na vibarua kama ilivyo Kwa sasa katika viwanda," alisema.
Pia aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwapatia ajira watanzania zaidi 100 kufanya kazi katika kiwanda hicho.
Alisema uongozi wa kiwanda hicho unawajali wazawa ambapo kati ya wafanyakazi 144 ni watanzania na sita ni wakutoka nje ya nchi.
Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano kuhamasisha Tanzania kuwa ya viwanda,kwa sasa wamejikita kusambaza umeme wa gesi ili kuviwezesha viwanda kutolipa gharama kubwa kwa matumizi ya nishati hiyo.
Alitoa wito kwa vijana kuvilinda viwanda vinavyoanzishwa katika maeneo yao na sio kuiba mali za viwanda hivyo.
" Wapo vijana sio waaminifu badala ya kuvisimamia viwanda viwasaidie katika vijiji,lakini wao ndio hao wanaogeuka kuihujumu miundombinu," alisema
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.