Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga yataoa mafunzo kwa vikundi ambavyo vinatarajia kupewa Mkopo wa 10%
Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku 3 ambayo yanaratibiwa na idara ya maendeleo ya Jamii yenye lengo la kuwaelimisha juu ya usimamizi na uendeshaji miradi yenye tija ili waweze kurejesha fedha za mikopo waliyopewa.
Jumla ya kiasi cha shilingi Mil.94,967,000 zinatarajiwa kutolewa kwa vikundi 4 vyenye wanaufaika 17 kati ya wanawake 6 na wanaume 11.
Katika mafunzo hayo kulikuwa na mada ambazo utatuzi wa migogoro ya vikundi,usimamizi wa biashara,kuweka akiba na usimamizi wa fedha na mali za kikundi,mkataba na taratibu za urejeshaji wa mikopo na taratibu za ununuzi wa vifaa na uendeshaji wa vyombo vya usafiri.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.