Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mh. Hadija Nassir Ali amempongeza Mkurugenzi Mtendanji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kwa kusimamia vyema sera ya Serikali ya kutoa mikopo ya asilimia kumi fedha zinazotokana na mapato ya ndani.
Akizungumza na wanufaika wa mikopo hiyo wakati wa mafunzo yanayoendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Resouce Centre kiguza Ndg. Clement Muya kaimu Mkuu wa Wilaya na Afisa Tarafa ya Mkuranga amesema katika kipindi cha Miaka Mitano iliyopita Halmashauri imetoa fedha kiasi cha shilingi Bil. 1.6 kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu ikiwa na lengo la kusaidia jamii kuondokana na umasikini.
Akiendelea Kaimu Mkuu wa wilaya aliwaambia vijana kutumia fedha hizo kwa ajili ya malengo waliyojiwekea kwenye vikundi na sio kugawana kama ambavyo makundi mengi yamekua yakifanya.
Nae Mkurugenzi Mtendani Bi. Mwantumu Mgonja amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga itaendelea kutekeleza sheria ya fedha ya Serikali za mitaa ya mwaka (2018) pamoja na kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo za mwaka (2019) ambazo zimeelekeza mamlaka za serikali za mitaa kutenga asilimia kumi ya mapato yake wanayokusanya kutoka kwenye vyanzo vya ndani vya mapato.
Akiwasilisha taarifa za utoaji mikopo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Mwanamsiu Dossi amesema kwa kipindi cha kuanzia Mwezi mei 2021/2022 Halmashauri itatoa jumla ya Tsh. Mil. 208,973,000 kwa vikundi 24 vya wajasiliamali,
Aidha amesisitiza kuwa Mikopo iliyotolewa ni kiasi cha shilingi 105,365,000 kwa vikindi 15 vya wanawake na Shilingi 103,608,000kwa vikundi 9 vya vijana.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.