Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi imeendesha mafunzo kwa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki katika vituo vitatu wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Mafunzo hayo yanayohusu uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura limetanguliwa na zoezi la kuapishwa kiapo cha kutunza siri kwa waandikishaji hao ambapo baadae wataendeelea na mafunzo ya kutumia vifaa hivyo.
Aidha Mafunzo hayo kwa Mkuranga yanafanyika katika Chuo cha ualimu Vikindu, ukumbi wa Flex Garden na katika shule ya Perfect destiny Mkuranga yameanza tarehe 10 Februeri 2025 na yanatarajia kukamilika tarehe 11 Februari 2025.
Zoezi la uandikishaji Mwaka huu limebebwa na kauli mbiu isemayo "Kujiandikisha kuwa Mpiga kura, ni Msingi wa Uchaguzi Bora"
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.