Wadau wa korosho ndani ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wametakiwa kuzingatia kanuni , mwongozo na sheria ili zao hilo liendelee kuchangia kuboresha maisha yao na kukuza uchumi wa Halmashauri ya Wilaya.
Akifungua kikao hicho leo Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao Filberto Sanga aliviagiza vyama vya msingi vya wakulima (AMC0S) kuhakikisha wanachagua viongozi watakaojali maslahi ya wakulima.
Sanga akifafanua zaidi alisema changamoto kubwa ni uteuzi wa makatibu wa vyama hivyo ambao sio wakazi wa maeneo husika na kutokuwa na elimu ya kidato cha nne haliinayochangia wakulima wakose haki zao za msingi ikiwemo malipo ya korosho zao.
Kiongozi huyo alitumia fursa hiyo kuwataka wakulia waache utamaduni wa kuchoma mashamba baada ya kusafisha hali inayopunguza thamani sambamba na kutokutunza korosho majumbani badala ya kwenye maghala.
Mwenyekiti huyo alimtaka mwakilishi wa bodi ya korosho Tanzania (CBT)Jafari Matata, na chama kikuu cha ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU) kuwachunguza na kuwasimamia wanunuzi wakidhi vigezo ili kuhakikisha wakulima wanapata malipo mazuri kulingana na ubora halisi wa korosho.
Kikao hicho kilichomshirikisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde , wataalamu na watendaji kimepanga mikakati ili kuhakikisha changamoto za msimu uliopita hazijirudii tena.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.